Maktaba ya Nukuu za Marais Tanzania
Historia • Fikra • Uongozi • Kumbukumbu
Benjamin William Mkapa
Kuhusu

Benjamin
William Mkapa

1938 — 2020

Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwanadiplomasia, mwandishi wa habari na kiongozi aliyohudumu katika kipindi muhimu cha mageuzi ya Tanzania ya miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Alizaliwa
12 Novemba 1938
Masasi, Mtwara
Urais
1995 — 2005
Rais wa Tanzania
Elimu
Makerere University
Columbia University
Alifariki
23 Julai 2020
Dar es Salaam
Wasifu

Maisha na Utumishi

Benjamin William Mkapa (1938–2020) alikuwa Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mmoja wa viongozi muhimu katika historia ya Tanzania ya baada ya uhuru. Aliiongoza nchi kuanzia mwaka 1995 hadi 2005, katika kipindi kilichoshuhudia mageuzi katika uchumi, utawala, diplomasia na nafasi ya Tanzania katika jumuiya ya kimataifa.

Alikuwa pia Rais wa kwanza wa Tanzania kuchaguliwa katika mfumo wa vyama vingi baada ya kurejeshwa kwa mfumo huo mwaka 1992.

Mkapa alizaliwa 12 Novemba 1938 huko Masasi, Mkoa wa Mtwara, na alipata elimu yake ya msingi na sekondari katika shule mbalimbali nchini Tanzania. Mwaka 1962 alipata shahada ya Bachelor of Arts katika Kiingereza kutoka Makerere University College nchini Uganda. Baadaye alisoma masuala ya diplomasia na uhusiano wa kimataifa katika Columbia University nchini Marekani.

Alianza utumishi wa Serikali mwaka 1962 kama Afisa Tawala mjini Dodoma na baadaye akawa Afisa Mambo ya Nje. Kuanzia miaka ya 1960 alijenga pia taaluma ndefu katika uandishi wa habari na uhariri, akihudumu katika vyombo mbalimbali vya habari, ikiwemo The Nationalist, Uhuru, Daily News na Sunday News.

Mwaka 1974 aliteuliwa kuwa Afisa Habari wa Rais, na mwaka 1976 akawa mhariri mwanzilishi wa Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA).

Mana ya uongozi ni kuwajali watu na kuwapa fursa ya maisha bora.
Benjamin William Mkapa
Historia

Matukio Muhimu ya Maisha
na Uongozi

1938

Kuzaliwa Masasi

Benjamin William Mkapa alizaliwa tarehe 12 Novemba 1938 huko Masasi, Mkoa wa Mtwara.

1962

Shahada ya Chuo Kikuu

Alipata shahada ya Bachelor of Arts katika Kiingereza kutoka Makerere University College nchini Uganda.

1976

Balozi wa Tanzania nchini Nigeria

Aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na kuendelea na safari yake ya kidiplomasia.

1995

Rais wa Tanzania

Alishinda uchaguzi wa mwaka 1995 na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2000

Kuchaguliwa tena

Alishinda uchaguzi wa mwaka 2000 na kuendelea na kipindi chake cha pili cha uongozi.

2005

Kukabidhi Madaraka

Tarehe 21 Desemba 2005 alikabidhi madaraka baada ya kumaliza vipindi vyake viwili vya urais.

2020

Kifo

Alifariki tarehe 23 Julai 2020 jijini Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 81.

Benjamin William Mkapa akihutubia katika Umoja wa Mataifa
Kumbukumbu ya Kimataifa

Mkapa katika jukwaa la kimataifa

Picha hii inaonesha sehemu ya safari ya Benjamin William Mkapa katika diplomasia na uhusiano wa kimataifa, ikiwa ni mojawapo ya picha zenye uzito wa kumbukumbu katika historia yake ya utumishi.

Benjamin William Mkapa katika shughuli ya kimataifa. Picha imehifadhiwa katika mkusanyiko wa picha wa Maktaba ya Nukuu za Marais Tanzania.
Uongozi wa Taifa

Kipindi cha Urais
1995 — 2005

Alipoingia madarakani mwaka 1995, Tanzania ilikuwa katika kipindi cha mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa. Uongozi wake uliendelea na mageuzi ya kiuchumi yaliyoanza katika miaka iliyotangulia, huku ukisisitiza nidhamu ya fedha za Serikali, mageuzi ya taasisi za umma, kuvutia uwekezaji na kuongeza ushiriki wa Tanzania katika uchumi wa kimataifa.

Kipindi chake kilihusishwa pia na juhudi za kupunguza umaskini na kuimarisha huduma za kijamii na utawala.

Katika uwanja wa kisiasa, Mkapa aliongoza Tanzania katika miaka ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi. Alishinda uchaguzi wa mwaka 1995 na kuchaguliwa tena mwaka 2000, hivyo kuhudumu kwa vipindi viwili vya miaka mitano.

Tarehe 21 Desemba 2005, alikabidhi madaraka baada ya kumaliza vipindi vyake viwili vya urais, na kumrithisha madaraka Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Afrika na Dunia

Diplomasia na Urithi wa Kimataifa

Katika uwanja wa Afrika na diplomasia ya kimataifa, Mkapa alijenga urithi mpana zaidi ya mipaka ya Tanzania. Alihusika katika juhudi za amani na utatuzi wa migogoro barani Afrika, ushirikiano wa kikanda na mijadala ya maendeleo ya nchi zinazoendelea.

Baada ya kustaafu Urais, aliendelea kushiriki katika taasisi na majukwaa mbalimbali ya kimataifa, ikiwemo South Centre, ambako aliwahi kuwa Mwenyekiti.

Pia alishiriki katika juhudi za kimataifa kuhusu maendeleo, utandawazi na ushirikiano wa Afrika.

Urithi wa Kihistoria

Fikra, uongozi
na kumbukumbu

Urithi wa Benjamin William Mkapa katika historia ya Tanzania unaonekana katika kipindi cha uongozi kilichounganisha mageuzi ya kiuchumi, mfumo wa vyama vingi, diplomasia, utawala na ushirikiano wa kimataifa.

Historia yake haiwezi kutenganishwa na hatua ambazo Tanzania ilipitia katika kujenga uchumi wa kisasa, kuimarisha taasisi za Serikali na kujenga nafasi yake katika jumuiya ya kimataifa.

Mkapa katika Maktaba ya Nukuu

Kwa Maktaba ya Nukuu za Marais Tanzania, Benjamin William Mkapa ni mhusika muhimu katika kuelewa historia ya Tanzania ya miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Nukuu zake zinapaswa kusomwa kwa kuzingatia muktadha wa wakati zilipotolewa, hususan kuhusu uchumi, uwazi na ukweli, utawala, umaskini, demokrasia, diplomasia, Afrika na nafasi ya Tanzania katika dunia.

Kwa mtazamo huo, maktaba ya nukuu inaweza kuhifadhi si maneno ya Mkapa pekee, bali pia fikra na mazingira ya kihistoria yaliyoyazunguka.

Maktaba ya Nukuu za Marais Tanzania

Chagua Rais kutazama mkusanyo wa nukuu, kauli na fikra zake.

TAFUTA HAPA
NUKUU UITAKAYO
Andika neno kuu, mada au jina la Rais... Tafuta
Gundua hekima, maono na kauli za viongozi wa Tanzania
katika Maktaba ya Nukuu za Marais.
MAKTABA YA NUKUU
BENJAMIN WILLIAM MKAPA
Inapakia...
Benjamin William Mkapa
KUHUSU

BENJAMIN WILLIAM MKAPA

Benjamin William Mkapa (1938–2020) alikuwa Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mmoja wa viongozi muhimu katika historia ya Tanzania ya baada ya uhuru.

Aliiongoza Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005, katika kipindi muhimu cha mageuzi ya kiuchumi na kisiasa, kuimarika kwa diplomasia, mabadiliko katika utawala na kuongezeka kwa ushiriki wa Tanzania katika jumuiya ya kimataifa.

Mkapa alikuwa Rais wa kwanza wa Tanzania kuchaguliwa katika mfumo wa vyama vingi baada ya kurejeshwa kwa mfumo huo mwaka 1992. Uongozi wake ulihusishwa na mageuzi ya uchumi, nidhamu ya fedha za Serikali, mageuzi ya taasisi za umma, uwekezaji, kupunguza umaskini na kuimarisha nafasi ya Tanzania katika Afrika na dunia.

Kabla na baada ya Urais, Mkapa alijenga historia ndefu katika utumishi wa umma, uandishi wa habari, diplomasia na uongozi wa kimataifa. Urithi wake unaendelea kujadiliwa katika historia ya Tanzania, hususan katika masuala ya uchumi, demokrasia, utawala, uwazi, amani, diplomasia na maendeleo ya Afrika.

SOMA ZAIDI